“Hatuwezi kukubali leo hii wanawake waendelee kufa wakati wakijifungua.”
Malengo ya Milenia yaliyotangazwa mnamo Septemba 2000 yalikuwa hatua kubwa katika kuboresha afya ya akinamama na watoto duniani kote, hususani katika nchi zinazoendelea, ambako huduma hizi zinahitajika sana.
Katika kukubaliana na Malengo ya Milenia, wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa waliazimia vilivyo kutekeleza malengo haya ifikapo mwaka 2015. Jambo moja muhimu miongoni mwa malengo haya lilikuwa kupunguza kwa theluthi mbili vifo vya watoto wachanga wenye umri wa chini ya miaka mitano, na kupunguza kwa robo tatu vifo vya uzazi kwa akinamama.
soma zaidi


Swahili
English
Français
العربية

Hospitali ya Uzazi na Mafunzo ya Edna Adan iliyoko Hargeisa ilifunguliwa mwaka 2002 na Edna Adan Ismail kwa lengo la kutoa huduma za tiba kwa wanawake na watoto. Hospitali hii ni kituo kimoja kati ya vituo viwili nchini Somaliland vinavyotoa mafunzo kwa wakunga na wauguzi.



